Al-A'raaf 7:194
الأعرافإِنَّ ٱلَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَٱدْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا۟ لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu nyinyi. Basi waombeni, nao wawaitikie ikiwa nyinyi ni wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika hao mnao waomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu nyinyi. Hebu waombeni, nao wakuitikieni, kama mnasema kweli. [194]
[194] Hakika hao mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, na mkataraji nafuu kwao, wao wenyewe wanamnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa hukumu ya maumbile yao. Kwani Yeye Mwenyezi Mungu amewafanya wafuate amri yake mfano wenu nyinyi. Kama nyinyi mnasema kweli katika madai yenu kuwa hao wanaweza lolote, basi watakeni, na wao wakutimilizieni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika wale ambao mnawaabudu badala ya Allah Mtukufu, enyi washirikina, wamemilikiwa na Mola wao, kama mlivyomilikiwa nyinyi na Mola wenu. Basi iwapo nyinyi, kama mnavyodai, ni wakweli kwamba wao wanastahiki wafayiwe chochote kile cha ibada, waiteni wawaitikie. Iwapo watawaitikia na watawapatia matakwa yenu, mtakuwa ni wakweli, na isipokuwa hivyo, itakuwa wazi kwamba nyinyi ni warongo mnamzulia Allah Mtukufu uzushi mkubwa kabisa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net