Al-A'raaf 7:193
الأعرافوَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى ٱلْهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمْ ۚ سَوَآءٌ عَلَيْكُمْ أَدَعَوْتُمُوهُمْ أَمْ أَنتُمْ صَـٰمِتُونَ
Na mkiwaita kwenye uongofu, hawawafuati. Ni mamoja kwenu ikiwa mtawaita au mkae kimya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mkiwaita kwenye uwongofu, hawakufuateni. Ni mamoja kwenu ikiwa mtawaita au mkinyamaza. [193]
[193] Na nyinyi mnao yaabudu masanamu! Mkiyaomba hayo masanamu yakuongozeni mpate mnacho kipenda hayakuitikieni hayo myatakayo! Ni sawa sawa kwenu kuwa hapana faida ya kuwaomba au mkinyamaza. Hali yao haibadiliki vyo vyote vile.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mnapowalingania, enyi washirikina, masanamu hawa ambao mliwaabudu badala ya Allah Mtukufu kwenye uongofu, hawasikii ulinganizi wenu wala hawawafuati nyinyi; inalingana sawa kuwalingania au kuwanyamazia. Kwani wao hawasikii wala hawaoni wala hawaongozi wala hawaongozwi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net