Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 192

Al-A'raaf 7:192

الأعراف

وَلَا يَسْتَطِيعُونَ لَهُمْ نَصْرًا وَلَآ أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ

Maana

Wala hawawezi kuwanusuru wala wao wenyewe hawajinusuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala hawana uwezo wa kuwanusuru wala wenyewe hawajinusuru. [192]

[192] Wala hayawezi kuwasaidia hao wanayo yaabudu, wala hayajisaidii wenyewe akitokea mtu kuyashambulia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala hawawezi kuwanusuru wenye kuwaabudu au kuzilinda nafsi zao na ubaya. Iwapo wao hawaumbi kitu, bali wao wameumbwa na hawawezi kuwalinda wanaowaabudu, wasipatikane na mambo wanayoyachukia, wala kuzilinda nafsi zao. Basi vipi wanafanywa ni waungu? Huu haukuwa isipokuwa ni upeo wa udhalimu na upeo wa uchache wa akili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net