Al-A'raaf 7:189
الأعرافهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَٰحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا ۖ فَلَمَّا تَغَشَّىٰهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِۦ ۖ فَلَمَّآ أَثْقَلَت دَّعَوَا ٱللَّهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ ءَاتَيْتَنَا صَـٰلِحًا لَّنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ
Yeye ndiye aliyewaumba kutoka katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili ajitulize kwake. Na alipomuingilia, akabeba mimba nyepesi, akitembea nao. Anapokuwa mjamzito, wote wawili humwomba Mwenyezi Mungu, Mola wao Mlezi: Kama ukitupa mwana mwema hakika tutakuwa katika wanaoshukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu. Na anapo muingilia hubeba mzigo mwepesi, akitembea nao. Anapo kuwa mja mzito, wote wawili humwomba Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wao: Kama ukitupa mwana mwema tutakuwa katika wanao shukuru. [189]
[189] Yeye ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, aliye kuumbeni hapo mwanzo kwa nafsi moja. Na akajaalia katika nafsi ile ile mwenzie, na vizazi vyao vikaendelea kuwepo. Nanyi mlikuwa mume na mke. Basi alipo muingilia akachukua mzigo mwepesi, nayo ndio mimba changa, inapo kuwa kama pande la damu na pande la nyama. Mimba ikiwa nzito katika tumbo lake huyo mke, mume na mke humwomba Mola wao Mlezi wakisema: Wallahi, ukitupa mwana mzima asiye na ila katika umbo lake, tutakushukuru kwa neema yako.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yeye Ndiye ambaye Aliyewaumba nyinyi, enyi watu, kutokana na nafsi moja, nayo ni Ãdam, amani imshukie. Na akaumba kutokana na nafsi hiyo ya pili yake, nayo ni Ḥawa’, ili aliwazike naye na ajitulize. Alipomuingilia – makusudio ni jinsi ya mke na mume miongoni mwa kizazi cha Ãdam – alibeba maji mapesi, akainuka nayo na akakaa nayo mpaka mimba ikatimia. Kilipokaribia kipindi cha kuzaa kwake na akawa mzito, walimuomba, mume na mke, Mola wao, «Tunaapa lau utatupatia mwanadamu aliye sawa, aliye mwema, hakika tutakuwa ni wenye kukushukuru kwa kutupa mtoto mwema».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net