Al-A'raaf 7:190
الأعراففَلَمَّآ ءَاتَىٰهُمَا صَـٰلِحًا جَعَلَا لَهُۥ شُرَكَآءَ فِيمَآ ءَاتَىٰهُمَا ۚ فَتَعَـٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Basi alipowapa mwana mwema, wakamfanyia washirikina Mwenyezi Mungu katika kile kile alichowapa. Basi Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi anapo wapa mwana mwema, wanamfanyia washirikina Mwenyezi Mungu katika kile kile alicho wapa. Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao [190]
[190] Akisha wapa wakitakacho, huwafanya masanamu ndio washirika wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika ile zawadi yake ya ukarimu, kwa kuyatambikia kama kwamba ndio wanayashukuru. Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye anaye stahiki kushukuriwa. Yeye ametukuka, hawezi kuwa kama hiyo miungu yao ya kishirikina.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Alipowaruzuku, yule mume na mke, mtoto mwema walimfanyia Allah Mtukufu washirika katika mtoto yule ambaye Allah Mtukufu Alipwekeka katika kumuumba wakamfanya ni mja wa asiyekuwa Allah Mtukufu; Ametukuka Allah Mtukufu na Ametakasika na kila mshirika.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net