Al-A'raaf 7:188
الأعرافقُل لَّآ أَمْلِكُ لِنَفْسِى نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ ٱلْغَيْبَ لَٱسْتَكْثَرْتُ مِنَ ٱلْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِىَ ٱلسُّوٓءُ ۚ إِنْ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu, ningalitenda mema sana, wala ubaya usingenigusa. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri kwa kaumu wanaoamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu ninge jizidishia mema mengi, wala ovu lisinge nigusa. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri kwa watu wanao amini. [188]
[188] Waambie: Mimi siimilikii nafsi yangu kujiletea nafuu, wala kujikinga na madhara, ila Mwenyezi Mungu akipenda hayo. Hapo ndio hunipa mamlaka. Na lau kuwa mimi najua yale yaliyo fichikana kwangu, kama mnavyo dhani, basi ningeli kithirisha kila kheri, kwa kuwa ninajua sababu zake. Na ninge ilinda nafsi yangu na kila ovu, kwa kuyaepuka yanayo leta madhara. Mimi si chochote ila ni mwonyaji wa adhabu, na mbashiri wa thawabu, kwa kaumu wanayo iamini Haki na wanait'ii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, «Siwezi kuiletea mema nafsi yangu wala kuiepushia shari yenye kuifikia, isipokuwa iwapo Allah Mtukufu Alitaka. Na lau mimi ningalikuwa najua yaliyofichika ningalifanya njia ambazo najua kwamba zitaniongezea maslahi na manufaa na ningalijikinga na shari yenye kuwa kabla haijatukia. Mimi si yoyote isipokuwa ni mjumbe wa Allah Mtukufu, Amenituma kwenu, naogopesha mateso Yake na natoa bishara njema ya thawabu Zake kuwalipa watu wanaoamini kuwa mimi ni Mtume wa Allah Mtukufu na wakafuata sheria Yake kivitendo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net