Al-A'raaf 7:187
الأعرافيَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَىٰهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّى ۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَآ إِلَّا هُوَ ۚ ثَقُلَتْ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً ۗ يَسْـَٔلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِىٌّ عَنْهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ ٱللَّهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Wanakuuliza kuhusu hiyo Saa (ya Kiyama) kusimama kwake ni lini? Sema: Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake isipokuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitawajia isipokuwa kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Elimu yake iko tu kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wa watu hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haikujiini ila kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini aghlabu ya watu hawajui. [187]
[187] Ewe Muhammad! Mayahudi wanakuuliza khabari ya Saa itakayo malizikia dunia. Itakuwa wakati gani, kujuulikana khasa? Waambie: Ujuzi wa wakati wake uko kwa Mwenyewe Mola wangu Mlezi peke yake. Haujui wakati wake mtu yeyote isipo kuwa Yeye. Itapo tokea kitisho chake kitakuwa kikuu kwa walioko mbinguni na ardhini! Wao wanakuuliza suala hili kama kwamba wewe una pupa ya kuijua! Basi wakaririe jawabu, na uwambie kwa kutia mkazo: Hakika kuijua hiyo Saa kuko kwa Mwenyezi Mungu, lakini aghlabu ya watu hawatambui hakika ya wasiyo yaona au wanayo yaona!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanakuuliza, ewe Mtume, makafiri wa Makkah kuhusu Kiyama: kusimama kwake ni lini? Waambie, elimu ya kusimama kwake iko kwa Allah Mtukufu, haitoi nje isipokuwa Yeye, imekuwa nzito kuijua na imefichika kwa watu wa mbinguni na ardhini. Hakuna Malaika aliyekaribishwa wala Mtume aliyetumilizwa anayejua wakati wa kusimama kwake. Hakiji isipokuwa kwa ghafla. Hawa watu wanakuuliza kuhusu hiko Kiyama kama kwamba wewe una pupa la kukijua, una bidii sana ya kukiuliza. Waambie, «Ujuzi wake uko kwa Allah Mtukufu Ambaye Anayajua yaliyofichika kwenye mbingu na ardhi. Lakini wengi wa watu hawajui kwamba hilo hakuna anayelijua isipokuwa Allah Mtukufu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net