Al-A'raaf 7:184
الأعرافأَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا۟ ۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ
Je, hawafikirii? Huyu mwenzao hana wazimu. Yeye siyo isipokuwa ni mwonyaji aliye dhahiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je, hawafikiri? Huyu mwenzao hana wazimu. Hakuwa yeye ila ni mwonyaji aliye dhaahiri. [184]
[184] Wao wameanza kwa kukadhibisha, wala hawakuzingatia yale anayo waitia kwayo Mtume, na hoja anazo zitoa. Bali wakamsingizia kuwa ni mwendaazimu, na hali hana wazimu chochote. Yeye huyu ni mwenye kuwaonya wasifikiwe na adhabu ya ushirikina wao. Na onyo lake liwazi, la dhaahiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hawafikirii hawa ambao walizikanusha aya zetu wakazingatia kwa akili zao na wakajua kwamba Muhammad hana wazimu? Yeye hakuwa isipokuwa ni mwenye kuwaonya wao mateso ya Allah Mtukufu kwa kumkanusha kwao Yeye, iwapo hawataamini, na ni mshauri muaminifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net