Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 183

Al-A'raaf 7:183

الأعراف

وَأُمْلِى لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِى مَتِينٌ

Maana

Nami nitawapa muda. Hakika mpango wangu ni madhubuti.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nami nitawapa muda. Hakika mpango wangu ni madhubuti. [183]

[183] Nitawakunjulia maisha, bila ya kuyapuuza maovu yao. Na mipango yangu niliyo wapangia ni ya nguvu na mikali juu yao, inalingana na madhambi yao yaliyo zidi kwa kupita kiasi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na nitawapa muhula hawa ambao walizikanusha aya zetu mpaka wadhanie kwamba wao hawatateswa, waongeze ukafiri na uasi. Na kwa hivyo, waongezewe adhabu. Kwani vitimbi vyangu ni vigumu, yaani: ni vya nguvu na vikali havizuiliwi kwa nguvu wala kwa hila.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net