Al-A'raaf 7:182
الأعرافوَٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ
Na wale waliokadhibisha Ishara zetu, tutawapeleka katika maangamio pole pole kutokea pale wasipojua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale walio kadhibisha Ishara zetu, tutawapururia pole pole kwa namna ambayo wenyewe hawaijui [182]
[182] Na wale walio zikanusha Ishara (Aya) zetu zilio teremshwa tutawapururia pole pole, na tutawawacha mpaka wafike ukomo watapo fika. Na hayo ni kwa kuwapururia neema juu yao, juu ya kushughulika kwao katika maasi, mpaka maangamizo yawazukie nao wameghafilika wakitaladhadhi na starehe zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale ambao walizikanusha aya zetu wakazikataa na wasiwaidhike nazo, tutawafungulia milango ya riziki na njia za maisha katika ulimwengu, kwa kuwavuta kidogo kidogo mpaka wahadaike kwa yale ambayo wako nayo na waitakidi kuwa wao wako kwenye kitu cha maana, kisha tutawatesa kwa ghafla kwa namna wasioijua. Haya ni mateso yatokayo kwa Allah Mtukufu ya kukanusha hoja za Allah Mtukufu na aya Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net