Al-A'raaf 7:181
الأعرافوَمِمَّنْ خَلَقْنَآ أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِٱلْحَقِّ وَبِهِۦ يَعْدِلُونَ
Na katika wale tuliowaumba wako umma wanaoongoza kwa haki, na kwayo wanafanya uadilifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika tulio waumba wako watu wanao ongoza kwa Haki, na kwayo wanafanya uadilifu. [181]
[181] Na katika tulio wajaalia waingie Peponi wapo wanao waita wengineo kwenye Haki kwa kuipenda Haki, na kwa Haki tu wanafanya uadilifu katika hukumu zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa wale tuliowaumba kuna kundi la watu bora wanaoongoka kwenye haki na wanaita watu waifuate, na kwa hiyo wanahukumu na wanafanyia watu uadilifu; na wao ni viongozi wa uongofu, kati ya wale ambao Allah Mtukufu Amewaneemesha kwa Imani na kufanya amali njema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net