Al-A'raaf 7:185
الأعرافأَوَلَمْ يَنظُرُوا۟ فِى مَلَكُوتِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَىْءٍ وَأَنْ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَدِ ٱقْتَرَبَ أَجَلُهُمْ ۖ فَبِأَىِّ حَدِيثٍۭ بَعْدَهُۥ يُؤْمِنُونَ
Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi, na vile vyote alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika vitu, na kwamba huenda muda wao umekwishakaribia? Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi, na vitu alivyo viumba Mwenyezi Mungu, na pengine ajali yao imekwisha karibia? Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?. [185]
[185] Wamemwambia Muhammad mwongo kwa Tawhidi anayo waitia, wala hawakutazama kwa kuzingatia na kutafuta dalili za ufalme mtukufu wa Mwenyezi Mungu ulioko katika mbingu na ardhi na viliomo ndani yao, zinazo onyesha ukamilifu wa uwezo wa huyu Mwenye kuunda, na zinazo onyesha Umoja wake wa pekee. Wala hawakufikiri kuwa ajali yao imekwisha karibia, au huenda ikawa imekaribia, wapate kufanya haraka kutupia nadhari na kuitafuta Haki kabla ya kuzuka ajali. Ikiwa basi watu hawa hawaamini maneno ya Qur'ani watakuja amini maneno gani baada yake
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au kwani hawaangalii, hawa wakanushaji aya za Allah Mtukufu, kwenye ufalme wa Allah Mtukufu uliyo mkubwa na mamlaka Yake yenye uwezo wa kushinda, mbinguni na ardhini na chochote kile Alichokiumba Allah Mtukufu, zimetukuka sifa Zake, kwenye vitu viwili hivyo, wakalitia akilini hilo na wakalizingatia kwa akili zao na wakaangalia muda wa kikomo cha maisha yao ambao huenda ukawa umesongea karibu wakawa watakufa kwenye ukafiri wao na watakuwa kwenye adhabu ya Allah Mtukufu na mateso yake makali? Basi ni kitisho gani na onyo gani baada ya onyo la Qur’ani wataliamini na watalifanyia kazi?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net