Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 178

Al-A'raaf 7:178

الأعراف

مَن يَهْدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلْمُهْتَدِى ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ

Maana

Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, basi huyo ndiye mwongofu. Na yule aliyempoteza, basi hao ndio waliohasiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yule ambae Mwenyezi Mungu amemuhidi (amemuongoza) basi huyo amehidika (ameongoka) na alie muacha kupotea basi hao ndio walio Khasirika [178]

[178] Na yule ambaye Mwenyezi Mungu amemwezesha kufuata njia ya haki huyo basi ndie aliye ongoka kweli, mwenye kupata furaha ya kote kuwili duniani na Akhera. Na mwenye kukosa uwezesho huo kwa sababu ya kumilikiwa na pumbao lake basi watu hao ndio walio khasiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yule ambaye Allah Mtukufu Anamuafikia kumuamini Yeye na kumtii, huyo ndiye aliyeafikiwa; na yule ambaye Anamuachilia hampi taufiq, huyo ndiye mwenye hasara, mwenye kuangamia. Kuongoza na kupoteza kunatokana na Allah Mtukufu Peke Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net