Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 177

Al-A'raaf 7:177

الأعراف

سَآءَ مَثَلًا ٱلْقَوْمُ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا وَأَنفُسَهُمْ كَانُوا۟ يَظْلِمُونَ

Maana

Mfano mbaya zaidi ni wa kaumu waliozikadhibisha Ishara zetu na walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Huu ni mfano muovu kabisa wa watu wanao kanusha Ishara zetu na wakajidhulumu nafsi zao. . [177]

[177] Ni mbaya kweli hali ya hao wanao zipinga Ishara zetu, na kwa huku kukengeuka kwao na kuacha Haki hakumdhulumu mtu ila nafsi zao tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni mfano mbaya ulioje! Mfano wa watu waliokanusha hoja za Allah Mtukufu na dalili Zake wakazikataa na hali kwamba ni nafsi zao wenyewe walikuwa wakizidhulumu kwa sababu ya kukanusha kwao hoja hizi na dalili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net