Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 176

Al-A'raaf 7:176

الأعراف

وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَـٰهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُۥٓ أَخْلَدَ إِلَى ٱلْأَرْضِ وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ ۚ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ ٱلْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا ۚ فَٱقْصُصِ ٱلْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

Maana

Na lau kuwa tungelitaka, tungelimwinua kwazo, lakini yeye alizama katika ulimwengu na akafuata matamanio yake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi nje, na ukimwacha, pia hupumua na kutoa ulimi nje. Huo ni mfano wa kaumu ambao walizikadhibisha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tungelitaka tungeli mtukuza kwa hizo Ishara, lakini yeye aliushikilia ulimwengu na akafuata pumbao lake. Basi mfano wake ni mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi na ukimwacha pia hupumua na kutoa ulimi. Huo ni mfano wa kaumu wanao zikanusha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari. [176]

[176] Na lau tungeli taka kumnyanyua afike daraja za watu wema, tungeli mnyanyua kwa kumwezesha kuyatenda maamrisho ya hizo Aya.. Lakini yeye alishikamana na dunia, na hakuweza kunyanyuka kwendea uwingu wa uwongofu. Akafuata matamanio yake. Akawa hali yake daima yumo katika dhiki, na kushughulika kwake ni kwa dunia, na tafakuri zake duniani ni kutaka kuipata hiyo dunia basi. Hali yake ni kama hali ya mbwa anapo kuwa katika hali ovu kabisa, anavyo kuwa daima anapumua na kutoa limi lake nje, ukimkemea au ukimwacha. Hudorora ulimi wake kwa kuvuta pumzi kwa shida! Kadhaalika mwenye kuipenda dunia hudumu daima katika kuwania starehe zake na matamanio yake! Hakika hizo ndizo sifa zinazo mueleza huyo mwenye kuziacha Aya zetu, na ndio sifa ya wote wanao zikadhibisha Aya zetu zilio teremka. Basi wasimulie kisa chake hichi, huenda wakafikiri na wakaamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau tungetaka kukitukuza cheo chake kwa aya tulizompa tungalifanya, lakini yeye alitegemea ulimwengu na akafuata matamanio yake, na akafadhilisha ladha zake na hawaa zake juu ya Akhera, na akakataa kumtii Allah Mtukufu na akaenda kinyume na amri Yake. Mfano wa mwanamume huyu ni mfano wa mbwa: ukimfukuza au ukimuacha hutoa ulimi wake katika hali zote mbili. Basi hivyo ndivyo alivyo yule aliyejivua aya za Allah Mtukufu kwa kuziacha, huwa akiendelea katika ukafiri wake ikiwa utafanya bidii kumlingania au utampuuza. Sifa hii, ewe Mtume, ndiyo sifa ya watu hawa waliokuwa wapotevu kabla hujawajia kwa uongofu na utume. Basi simulia, ewe Mtume, habari za watu waliopita, kwani katika kutolea kwako habari zao ni miujiza mikubwa zaidi; na huenda watu wako wakazingatia juu ya yale uliyowajia nayo na wakakuamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net