Al-A'raaf 7:175
الأعرافوَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ٱلَّذِىٓ ءَاتَيْنَـٰهُ ءَايَـٰتِنَا فَٱنسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ ٱلشَّيْطَـٰنُ فَكَانَ مِنَ ٱلْغَاوِينَ
Na wasomee habari za yule ambaye tulimpa Ishara zetu, naye akajivua kutoka kwazo, basi Shetani akamfuata. Kwa hivyo, akawa miongoni mwa waliopotea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wasomee khabari za yule ambaye tulimpa Ishara zetu, naye akajivua nazo. Na Shet'ani akamuandama, akawa miongoni walio potea. [175]
[175] Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa wanao kadhibisha kwa Aya zake alizomteremshia Mtume wake. Akasema: Ewe Nabii! Wasomee kaumu yako khabari za mtu mmoja katika Wana wa Israili. Tulimpa ilimu ya kuzijua Ishara tulizo wateremshia Mitume wetu. Yeye huyo akazipuuza, wala asizishughulikie. Basi Shetani akamfuata kwa khatua zake, na akamtawala kwa upotovu wake, akawa katika kundi la walio potea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wasimulie,ewe Mtume, watu wako habari ya mwanamume mmoja miongoni mwa Wana wa Isrãîl, tuliyompa hoja zetu na dalili zetu, akajifunza hizo kisha akazikanusha na akazitupa nyuma ya mgongo wake, akashindwa na Shetani na akawa ni miongoni mwa wapotevu wenye kuangamia, kwa sababu ya kuenda kinyume kwake na amri ya Mola wake na kumtii kwake Shetani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net