Al-A'raaf 7:174
الأعرافوَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ وَلَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Na ndiyo kama hivyo tunavyozieleza Ishara kwa kina, ili huenda wakarejea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ndio kama hivyo tunavyo zipambanua Ishara, kwa kutaraji kuwa watarejea. [174]
[174] Kwa mfano wa maelezo wazi yenye hikima tunawabainishia wanaadamu dalili za kuwepo Mwenyezi Mungu, ili warejee waache ukhalifu wao na kuwafuata wapotovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kama tulivyozipambanua hizo aya na tukaeleza ndani yake tulichowafanyia watu waliopita, ndivyo tunavyozipambanua aya na kuzieleza kwa watu wako, ewe Mtume, kwa kutazamia kwamba watarudi waache ushirikina wao na warajee kwa Mola wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net