Al-A'raaf 7:179
الأعرافوَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ ءَاذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَآ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ كَٱلْأَنْعَـٰمِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْغَـٰفِلُونَ
Na hakika tumeiumbia Jahannamu wengi katika majini na watu. Wana nyoyo wasizofahamu kwazo. Na wana macho wasiyoona kwayo. Na wana masikio wasiyosikia kwayo. Hao ni kama wanyama wa mifugo, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tumeiumbia Jahannamu majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika. [179]
[179] Na tumewaumbia wengi katika majini na watu marejeo yao ni Motoni Siku ya Kiyama. Kwani hao wana nyoyo zisio funguka ikaingia Haki ndani yake. Wana macho yasiyo angalia dalili za kudra. Wana masikio yasiyo sikia Aya na mawaidha kwa sikio la kuzingatia na kuwaidhika! Hao ni kama wanyama kwa kutonafiika kwa neema ya akili za kuzingatia walizo neemeshwa na Mwenyezi Mungu. Bali hao ni wapotovu zaidi kuliko wanyama, kwani wanyama hutaka cha kuwafaa na hukimbia cha kuwadhuru. Lakini hawa watu hata hawatambui hayo. Hao ndio walio fikia ukomo wa kughafilika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika tuliuumbia Moto - ambao ndani yake Allah Mtukufu Atawaadhibu wanaostahili kuadhibiwa huko Akhera- majini na binadamu wengi, wana nyoyo lakini hawaelewi kwazo, hawatazamii malipo mazuri wala hawaogopi mateso; na wana macho hawaangalii kwayo aya za Allah Mtukufu na dalili Zake, na wana masikio hawasikii kwayo aya za Kitabu cha Allah Mtukufu na kuzitia akilini. Hawa ni kama wanyama wasioelewa waambiwacho, wasiofahamu wakionacho na wasiotia akilini kwa nyoyo zao kizuri na kibaya wakaweza kuzitenganisha. Bali wao wamepotea zaidi kuliko hao wanyama, kwani wanyama wanaona yanayowafaa na yanayowadhuru na wanamfuata mchungaji wao. Ama wao ni kinyume cha hilo, wao ndio wenye kughafilika na jambo la kumuamini Allah Mtukufu na kumtii.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net