Al-A'raaf 7:171
الأعرافوَإِذْ نَتَقْنَا ٱلْجَبَلَ فَوْقَهُمْ كَأَنَّهُۥ ظُلَّةٌ وَظَنُّوٓا۟ أَنَّهُۥ وَاقِعٌۢ بِهِمْ خُذُوا۟ مَآ ءَاتَيْنَـٰكُم بِقُوَّةٍ وَٱذْكُرُوا۟ مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
Na pale tulipounyanyua mlima juu yao ukawa kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika, na wakadhani kuwa utawaangukia, (tukawaambia): Chukueni yale tuliyowapa kwa nguvu, na yakumbukeni yaliyo ndani yake ili mche.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pale tulipo unyanyua mlima juu yao ukawa kama kwamba ni kiwingu kilicho wafunika, na wakadhani kuwa utawaangukia, (tukawaambia): Kamateni kwa nguvu tuliyo kupeni, na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mpate kumcha Mungu. [171]
[171] Mwenyezi Mungu ameijibu kauli ya Mayahudi walipo sema kwamba Wana wa Israili hawakupata kwenda kinyume na Haki. Alisema: Ewe Nabii! Wakumbushe pale tulipo unyanyua mlima juu ya Wana wa Israili ukawa kama kiwingu, na wakafazaika kwa kuwa walidhani utawaangukia. Nasi tukawaambia wakati ule ulipo nyanyuliwa na wao wamo katika khofu: Yashikeni ya uwongofu tuliyo kupeni katika Taurati kwa nguvu na kuazimia ut'iifu. Na kumbukeni yaliyomo ndani yake ili mpate kuzingatia na zitengenee nafsi zenu kwa kuchamngu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tulipoliinua jabali juu ya Wana wa Isrãîl likawa kama kwamba ni kiwingu kinachowafinika, wakawa na yakini kuwa kitawaangukia iwapo hawatazikubali hukumu zilizomo kwenye Taurati, na tukawaambia, Chukueni tulichowapa kwa nguvu. Yaani, fuateni kivitendo tulichowapa kwa bidii yenu, na yakumbukeni yaliyomo kwenye Kitabu chetu ya ahadi na masharti tuliyoyachukuwa kwenu kwamba mtayatekeleza yaliyomo ndani yake, ili mumche Mola wenu mpate kuokoka na mateso Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net