Al-A'raaf 7:170
الأعرافوَٱلَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِٱلْكِتَـٰبِ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُصْلِحِينَ
Na wale wanaokikamata sawasawa Kitabu, na wakasimamisha Swala, hakika Sisi hatupotezi ujira wa watengenezao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale wanao kishikilia Kitabu, na wakashika Swala - hakika Sisi hatupotezi ujira wa watendao mema. [170]
[170] Na wanao ikamata baraabara Taurati, na wakashika Swala zilizo faridhiwa kwao, hakika Sisi hatutaupoteza ujira wao kwa sababu ya kutengeneza kwao na kutenda kwao mema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanaoshikamana na Kitabu, wanaoyafuata kivitendo yaliyomo ndani yake miongoni mwa mambo ya itikadi na hukumu na wanaodumu na Swala kwa mipaka yake na wasiozipoteza nyakati zake, Allah Mtukufu Atawalipa kwa matendo yao mema na hatayapoteza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net