Al-A'raaf 7:169
الأعراففَخَلَفَ مِنۢ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَـٰذَا ٱلْأَدْنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِن يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِّثْلُهُۥ يَأْخُذُوهُ ۚ أَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِم مِّيثَـٰقُ ٱلْكِتَـٰبِ أَن لَّا يَقُولُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلْحَقَّ وَدَرَسُوا۟ مَا فِيهِ ۗ وَٱلدَّارُ ٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Basi wakafuatia baada yao wafuatizi waliokirithi Kitabu. Wanachukua anasa za haya maisha duni, na wanasema, "Tutasitiriwa dhambi!" Na ikiwajia tena anasa mfano wake, wanaichukua pia. Je, halikuchukuliwa juu yao agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu? Nao wamekwishasoma yale yaliyo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wachao. Basi je, hamtii akilini?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakafuatia baada yao kizazi kibaya walio rithi Kitabu. Wakashika anasa za haya maisha duni, na wakasema: Tutasamehewa! Na ikiwajia tena anasa kama hiyo wataishika pia. Je, hawakufanyiwa agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila Haki tu? Nao wamekwisha soma yaliomo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wanao jikinga na maasi. Basi je, hamtii akilini? [169]
[169] Baada ya hao tulio kwisha wataja na tukawagawa sehemu mbili, walifuatia waovu wakairithi Taurati kutokana na walio watangulia. Lakini hao hawakufanya yalio amrishwa humo. Kwani wao walishika starehe ya dunia badala ya Neno la Haki. Wakijiambia nafsi zao: Mwenyezi Mungu atatusamehe kwa tunayo yatenda! Wakitaraji maghfira, na ilhali kuwa yakiwajia kama yale waliyo yashika watayashika vile vile. Basi wao wamekuwa wameshikilia kuendelea na madhambi pamoja na kutaka kwao msamaha. Tena basi Mwenyezi Mungu anawatahayarisha kwa vile kutaka maghfira na huku wanaendelea na yao, akasema: Sisi tulichukua kwao ahadi katika Taurati - nao wameyasoma yaliomo humo - kuwa waseme kweli; nao wakasema uwongo! Na hakika neema za nyumba ya Akhera za wanao jikinga na maasi ni bora kuliko starehe za duniani! Basi je, mtaendelea na uasi wenu, wala hayaingii akilini mwenu kuwa neema hizo ni bora kwenu? Na mnakhiari badala yake hizo starehe za dunia?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakaja, baada ya hawa ambao tulieleza sifa zao, watu ambao ni wabovu Walichukua Kitabu kutoka kwa wakale wao, wakakisoma na wakakijua, na wakaenda kinyume na hukumu zake, wakawa wanachukua kile wanacholetewa cha starehe ya ulimwenguni kinachotokana na njia mbaya za mapato kama hongo na mfano wake. Hayo ni kwa sababu ya wingi wa pupa lao na uroho wao, na wanasema pamoja na hayo, «Allah Mtukufu Atatusamehe,» wakitamani kwa Allah Mtukufu mambo yasiyofaa, na ikiwajia Mayahudi hawa starehe yenye kuondoka, miongoni mwa vitu vya haramu, huichukua na kuihalalisha, huku wakiendelea kufanya madhambi yao na kutumia haramu. Kwani hazikuchukuliwa kwao ahadi juu ya kuisimamisha Taurati na kufuata kivitendo yaliyomo ndani yake na kwamba hawatasema juu ya Allah Mtukufu isipokuwa ukweli na kwamba hawatamzulia urongo, wakayajua yaliyomo Kitabuni, wakayapoteza na wakaenda kinyume na ahadi ya Allah Mtukufu kwao katika hilo? Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanaomcha Allah Mtukufu, wakafuata amri Zake na wakaepuka makatazo Yake. Kwani hawa wanaochukua mapato duni hawaelewi kwamba yaliyo mbele ya Allah Mtukufu ni bora zaidi na yenye kusalia zaidi kwa wachamungu?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net