Al-A'raaf 7:168
الأعرافوَقَطَّعْنَـٰهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ أُمَمًا ۖ مِّنْهُمُ ٱلصَّـٰلِحُونَ وَمِنْهُمْ دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَبَلَوْنَـٰهُم بِٱلْحَسَنَـٰتِ وَٱلسَّيِّـَٔاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Na tukawagawanya katika ardhi umma mbalimbali. Miongoni mwao kuna wale walio wema, na miongoni mwao kuna walio kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mazuri na mabaya huenda wakarejea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tuliwafarikisha katika ardhi makundi makundi. Wako kati yao walio wema, na wengine kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mema na mabaya ili wapate kurejea. [168]
[168] Na Sisi tumewagawa makundi makundi duniani. Wamo kati yao walio wema. Na hao ndio walio amini wakenda mwendo ulio sawa. Na wapo miongoni mwao watu wasio sifika kwa wema. Na wote tumewafanyia mitihani kwa kuwapa neema na kuwapa nakama, ili watubu, waache waliyo katazwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwagawanya Wana wa Isrāîl makundi: kati yao kuna wanaosimama kutekeleza haki za Allah Mtukufu na haki za waja Wake, na kati yao kuna wenye kufanya kasoro wenye kuzidhulumu nafsi zao. Na hawa tuliwapa mtihani wa maisha ya neema na ukunjufu wa riziki; na pia tuliwapa mtihani wa maisha ya dhiki, misiba na matatizo kwa matarajio kuwa watarudi kumtii Mola wao na watatubia kutokana na vitendo vya kumuasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net