Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 172

Al-A'raaf 7:172

الأعراف

وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِنۢ بَنِىٓ ءَادَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا۟ بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَآ ۛ أَن تَقُولُوا۟ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَـٰفِلِينَ

Maana

Na pale Mola wako Mlezi alipochukua kutoka kwa wanadamu kutoka katika migongo yao dhuria zao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao (na kuwaambia), "Je, mimi si Mola wenu Mlezi?" Wakasema, "Ndiyo, tumeshuhudia." Mje mkasema Siku ya Kiyama, "Hakika sisi tulikuwa tumeghafilika mbali na haya."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo. [172]

[172] Hapa Mwenyezi Mungu amebainisha hidaya ya wanaadamu kwa kusimamisha dalili katika viumbe, baada ya kwisha bainisha kwa njia za Mitume na Vitabu. Alisema: Ewe Nabii! Waambie watu pale Mola wako Mlezi alipo watoa kutoka migongo ya wanaadamu na watoto wao na wanao zaliwa karne baada ya karne, kisha akwasimamishia dalili za Ungu wake, na akawapa akili na nadhari ya kuwawezesha kuzijua, na kwa hizo akili na nadhari waweze kutambua Tawhidi na Rubuubiya, yaani kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja Pekee na ni Mola Mlezi wa viumbe vyote, hata wakawa hao wanaadamu kama walio ulizwa: Je, Mimi siye Mola wenu Mlezi? Nao wakajibu: Kwani, Wewe ndiye Mola Mlezi wetu. Tunajishuhudia hayo juu ya nafsi zetu...Haya ni kwa kuwa kumkini kwao kupata kujua hizo hoja na dalili, na kutamakani kwao katika hayo imekuwa kama kwamba ni kukiri na kuungama. Na Sisi tumefanya haya ili msije kusema Siku ya Kiyama: Hakika sisi tulikuwa tumeghafilika na hiyo Tawhidi, na tulikuwa hatuijui. Katika Aya hii inaonyesha kuwa watoto asili yake wanatoka kwenye uti wa mgongo. Na ilimu ya kisasa imethibitisha kuwa kokwa za khaswa zinakuwa katika sehemu ya mgongo chini ya mafigo. Na zinakaa hapa mpaka katika miezi ya mwisho ya mimba ndio huteremka pale pahali pake pa kawaida panapo onekana. Na pengine hata hivyo huchelewa kuteremka hata baada ya mtoto kuzaliwa. Kadhaalika mayai ya mwanamke yanafanyika chini ya figo khasa, kisha ndio huteremka pahala pake karibu na tumbo la uzazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Mola wako Alipowatoa wana wa Ãdam kutoka kwenye migongo ya baba zao, Akawathibitishia upweke Wake kwa kuwatia tabia ya kimaumbile kwamba Yeye ni Mola wao, ni Muumba wao na ni Mmiliki wao; wakamkubalia hilo kwa kuchelea wasije kukanusha Siku ya Kiyama wasikubali chochote katika hilo na wasije wakadai kwamba hoja ya Allah Mtukufu haijasimama kwao na wala hawajui chochote juu yake, bali wao walikuwa wameghafilika na hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net