Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 165

Al-A'raaf 7:165

الأعراف

فَلَمَّا نَسُوا۟ مَا ذُكِّرُوا۟ بِهِۦٓ أَنجَيْنَا ٱلَّذِينَ يَنْهَوْنَ عَنِ ٱلسُّوٓءِ وَأَخَذْنَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ بِعَذَابٍۭ بَـِٔيسٍۭ بِمَا كَانُوا۟ يَفْسُقُونَ

Maana

Basi walipoyasahau yale waliyokumbushwa kwayo, tukawaokoa wale waliokuwa wakikataza mabaya, na tukawachukua wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya mno kwa vile walivyokuwa wakivuka mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi walipo yasahau waliyo kumbushwa, tuliwaokoa walio kuwa wakikataza maovu, na tukawatesa walio dhulumu kwa adhabu mbaya kwa vile walivyo kuwa wakifanya upotovu. [165]

[165] Walipo yaacha mawaidha waliyo pewa, tukawaokoa na adhabu wale ambao walikuwa wakikataza vitendo viovu, na tukwashika walio dhulumu na wakavuka mipaka na wakakhalifu kwa kuwapa adhabu kali, nayo ni udhalili na shakawa, kwa sababu ya kuendelea kwao kutokana na ut'iifu wa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi lilipoacha lile pote ambalo lilikiuka mipaka siku ya Jumamosi yale waliyokumbushwa na likaendelea kwenye upotevu wake na kukiuka mipaka kwake katika siku hiyo na lisiyakubali mawaidha waliyopewa na pote lenye kuwaidhia, Allah Mtukufu Aliwaokoa wale waliokuwa wanakataza maasia Yake na akawapatia wale waliokiuka mipaka siku ya Jumamosi adhabu kali mno kwa sababu ya kuenda kinyume kwao na amri ya Allah Mtukufu na kutoka kwao kwenye utiifu Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net