Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 166

Al-A'raaf 7:166

الأعراف

فَلَمَّا عَتَوْا۟ عَن مَّا نُهُوا۟ عَنْهُ قُلْنَا لَهُمْ كُونُوا۟ قِرَدَةً خَـٰسِـِٔينَ

Maana

Walipotakabari na kuasi yale waliyokatazwa, tukawaambia, "Kuweni manyani, mliodharauliwa."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walipo jifakharisha katika waliyo kanywa tuliwaambia: Kuweni manyani wa kudharauliwa. [166]

[166] Walipo zidi kuwa wagumu, na wakaendelea kutobali waliyo katazwa, wala adhabu kali isiwaachishe uovu, tukawafanya kama manyani kwa kuzigeuza nyoyo zao, na kuwaondolea uwezo wa kuifahamu Haki, wakawa mbali na kila kheri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi pote hilo lilipoasi na likayakiuka yale ambayo Allah Mtukufu Alioyakataza ya kutowinda siku ya siku ya Jumamosi, Allah Mtukufu Aliwaambia (watu wa pote hilo), «Kuweni manyani hali ni wanyoge ni wenye kuwekwa mbali na kila jema.» Na wakawa hivyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net