Al-A'raaf 7:164
الأعرافوَإِذْ قَالَتْ أُمَّةٌ مِّنْهُمْ لِمَ تَعِظُونَ قَوْمًا ۙ ٱللَّهُ مُهْلِكُهُمْ أَوْ مُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ قَالُوا۟ مَعْذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ
Na kikundi miongoni mwao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawaangamiza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola wenu Mlezi, na huenda nao wakamcha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamchamngu. [164]
[164] Na wakumbushe pia hao Mayahudi pale kikundi cha watu wema katika wenzao walio tangulia, ambao hawakutenda mabaya waliyo yatenda wengineo, walipo waambia wanao wapa mawaidha wale waovu: Kwa sababu gani mnawapa nasaha watu ambao Mwenyezi Mungu atawahiliki, au atawaadhibu adhabu kali Akhera, kwa sababu ya madhambi wanayo yatenda? Wakasema: Tunawapa mawaidha ili tupate udhuru kwa Mola wako Mlezi, tusiwe tumefanya taksiri, na kutaraji huenda wakamchamngu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi kundi kati yao waliposema kuwaambia kundi lingine lililokuwa likiwapa mawaidhia wale waliopita mipaka siku ya Jumamosi na likiwakataza wasimuasi Allah Mtukufu siku hiyo, «Kwa nini nyinyi mnawaidhia watu ambao Allah Mtukufu ni Mwenye kuwaangamiza ulimwenguni kwa kumuasi au ni Mwenye kuwaadhibu adhabu kali kesho Akhera?» Wakanena wale waliokuwa wakiwakataza wasimuasi Allah Mtukufu, «Tunawaidhia na tunawakataza ili tuwe na udhuru kuhusu wao na kwa ajili ya kutekeleza wajibu wa Allah Mtukufu juu yetu ya kuamrisha mema na kukataza maovu na kwa matumaini kwamba watamcha Allah Mtukufu, watamuogopa na watatubia kutokana na kumuasi kwao Mola wao na kupita mipaka ya mambo yaliyoharamishiwa kwao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net