Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 163

Al-A'raaf 7:163

الأعراف

وَسْـَٔلْهُمْ عَنِ ٱلْقَرْيَةِ ٱلَّتِى كَانَتْ حَاضِرَةَ ٱلْبَحْرِ إِذْ يَعْدُونَ فِى ٱلسَّبْتِ إِذْ تَأْتِيهِمْ حِيتَانُهُمْ يَوْمَ سَبْتِهِمْ شُرَّعًا وَيَوْمَ لَا يَسْبِتُونَ ۙ لَا تَأْتِيهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَبْلُوهُم بِمَا كَانُوا۟ يَفْسُقُونَ

Maana

Na waulize kuhusu kijiji kilichokuwa kando ya bahari, walipokuwa wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Walipokuwa samaki wakiwajia juu juu siku ya Sabato, na siku isiyokuwa ya Sabato hawawajii. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakivuka mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu. [163]

[163] Na waulize Mayahudi, kwa kuyachukia walio yafanya wenzao walio watangulia, khabari ya kijiji, nacho ni Elat, kilicho kuwa karibu na bahari. Wakaazi wake walivunja amri ya Mwenyezi Mungu ya kupiga marfuku kuvua samaki siku ya Jumaamosi, kuwa hiyo ni siku ya ibada tu kwao. Na siku hiyo samaki walikuwa wakiwajia vururu juu ya maji. Na siku isiyo kuwa Jumaamosi samaki walikuwa hawaji. Huo ni mtihani wa Mwenyezi Mungu! Na kwa mfano wa mtihani huo, au majaribio hayo yaliyo tajwa, ndio tunawajaribu kwa majaribio mengine kwa sababu ya upotovu wao unao endelea, ili adhihiri mwema na mbaya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na waulize, ewe Mtume, hawa Mayahudi kuhusu habari ya watu wa kijiji kilichokuwa karibu ya bahari, ambacho watu wake walikuwa wakipita mipaka siku ya Jumamosi kwa kufanya mambo yaliyoharamishwa na Allah Mtukufu, kwani Alikuwa Amewaamrisha waitukuze siku ya Jumamosi na wasivue samaki siku hiyo. Allah Mtukufu Akawajaribu na kuwapa mtihani, wakawa samaki wao wawajia siku ya Jumamosi kwa wingi wakiwa juu ya uso wa bahari, na Jumamosi ikipita wakawa samaki wanapotea na hawawaoni kabisa. Basi wakawa wafanya hila ya kuwatega siku ya Jumamosi kwenye mashimo na kuwavua baada yake. Na kama tulivyowaelezea vile Allah Mtukufu Alivyowajaribu na kuwapa mtihani kwa kuwatoa samaki juu ya bahari katika siku ambayo waliharamishiwa kuwavua na kuwaficha wasiwaone katika siku ambazo ni halali kwao kuwavua, ndivyo tunavyowafanyia mtihani wao kwa sababu ya uasi wao na kutoka kwao kwenye utiifu wa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net