Al-A'raaf 7:162
الأعراففَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مِنْهُمْ قَوْلًا غَيْرَ ٱلَّذِى قِيلَ لَهُمْ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِجْزًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُوا۟ يَظْلِمُونَ
Lakini wakabadilisha wale waliodhulumu miongoni mwao kauli isiyo ile waliyoambiwa. Basi tukawatumia adhabu kutoka mbinguni kwa vile walivyokuwa wakidhulumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini walio dhulumu miongoni mwao walibadilisha kauli, sio ile waliyo ambiwa. Basi tukawapelekea adhabu kutoka mbinguni kwa vile walivyo kuwa wakidhulumu. [162]
[162] Lakini waliikhalifu amri ya Mola wao Mlezi, wakasema kwa udhalimu maneno sio walio ambiwa, kwa kusudi ya kumkejeli Musa. Basi tukawateremshia adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya kuendelea kwao na udhalimu na kukiuka mpaka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waliomkanusha Allah Mtukufu kati yao waliligeuza neno ambalo Allah Mtukufu Aliwaamrisha waliseme, wakaingia mlangoni wakisota kwa makalio yao na wakasema, «ḥabbah fî sha‛rah» (mbegu kwenye unywele), hapo tukawateremshia adhabu kutoka mbinguni, tukawaangamiza kwayo, kwa sababu ya udhalimu wao na uasi wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net