Al-A'raaf 7:161
الأعرافوَإِذْ قِيلَ لَهُمُ ٱسْكُنُوا۟ هَـٰذِهِ ٱلْقَرْيَةَ وَكُلُوا۟ مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ وَقُولُوا۟ حِطَّةٌ وَٱدْخُلُوا۟ ٱلْبَابَ سُجَّدًا نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطِيٓـَٔـٰتِكُمْ ۚ سَنَزِيدُ ٱلْمُحْسِنِينَ
Na pale walipoambiwa: Ukaeni mji huu, na mle humo popote mpendapo, na semeni: 'Tufutie dhambi zetu.' Na uingieni mlango wake kwa kusujudu, tutawasitiria makosa yenu. Walio wema tutawazidishia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pale walipo ambiwa: Kaeni katika mji huu, na mle humo mpendapo, na semeni: Tufutie dhambi zetu. Na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu, tupate kukusameheni makosa yenu. Walio wema tutawazidishia. [161]
[161] Ewe Nabii! Wakumbushe hao waliopo miongoni mwao katika zama zako - ili iwe ni onyo kwa vile walivyo tenda walio watangulia - wakumbushe kauli yetu tulio waambia hao walio watangulia kwa ulimi wa Musa: Kaeni katika mji wa Baitul Muqaddas (Yerusalemu) baada ya kutoka jangwani. Na kuleni kheri zake kokote humo mtakako, na semeni: Tunakuomba ewe Mola Mlezi wetu, utufutie makosa yetu. Na muingie kwenye lango la mji kwa kuinamisha vichwa kama kurukuu kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu. Mkifanya hivyo tutakufutieni dhambi zenu, na tutazidisha thawabu za watendao mema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, uasi wa Wana wa Isrãîl kwa mola wao, kutakasika na sifa pungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, na Nabii wao Mûsã, amani imshukiye, na kugeuza kwao maneno waliyoamrishwa wayaseme pindi Alipowaambia Allah Mtukufu, kaeni mji wa Baitul Maqdis na kuleni matunda yake, nafaka zake na mimea yake popote mtakapo na wakati wowote mtakao na semeni, ‘tuondoshee dhambi zetu,’ na ingieni mlangoni mkimnyenyekea Allah Mtukufu, tutawasamehe makosa yenu na hatutawaadhibu kwayo, na tutawaongezea walio wema kheri mbili: za ulimwengu na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net