Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 156

Al-A'raaf 7:156

الأعراف

وَٱكْتُبْ لَنَا فِى هَـٰذِهِ ٱلدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِى ٱلْـَٔاخِرَةِ إِنَّا هُدْنَآ إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِىٓ أُصِيبُ بِهِۦ مَنْ أَشَآءُ ۖ وَرَحْمَتِى وَسِعَتْ كُلَّ شَىْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلَّذِينَ هُم بِـَٔايَـٰتِنَا يُؤْمِنُونَ

Maana

Na tuandikie mazuri katika dunia hii na katika Akhera. Hakika sisi tumerejea kwako. (Mwenyezi Mungu) akasema: Adhabu yangu nitamsibu kwayo nimtakaye. Na rehema yangu imeenea kila kitu. Basi nitaiandika hii hasa kwa wale wanaomcha Mungu, na wanaotoa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na utuandikie mema katika dunia hii na katika Akhera. Sisi tumerejea kwako. (Mwenyezi Mungu) akasema: Adhabu yangu nitamsibu nayo nimtakaye. Na rehema yangu imeenea kila kitu. Lakini nitawaandikia khasa wanao mchamngu, na wanao toa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu, [156]

[156] Na tukadirie hapa duniani maisha mema, na tupate tawfiqi tuweze kut'ii, na Akhera tupate malipo mazuri, na maghfira, na rehema, kwa kuwa sisi hakika tumekwisha rejea kwako na tunatubu kwako. Mola Mlezi wao akawaambia: Adhabu yangu namfikishia nimtakaye katika wasio tubu, na rehema yangu imeenea juu ya kila kitu, na nitawaandikia khasa wale wanao jikinga na ukafiri na maasi katika kaumu yako, na wanao toa Zaka zilio lazimishwa, na wanao sadiki Vitabu vyote vilivyo teremka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na utujaalie ni miongoni mwa wale uliowaandikia matendo mema ulimwenguni na Akhera. Sisi tumerejea kwako hali ya kutubia. Allah Mtukufu Akasema kumwambia Mûsã, Adhabu yangu nitampatiliza kwayo ninayemtaka miongoni mwa viumbe wangu, kama nilivyowapatiliza hawa niliowapatia katika watu wako, na rehema zangu zimewaenea viumbe wangu wote, nitawaandikia wale wanaomcha Allah Mtukufu na kuogopa mateso Yake, wakazitekeleza faradhi Zake na wakayaepuka mambo ya kumuasi, na wale ambao wao wanaziamini dalili za tawḥîd (kumpwekesha Allah Mtukufu) na hoja zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net