Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 154

Al-A'raaf 7:154

الأعراف

وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى ٱلْغَضَبُ أَخَذَ ٱلْأَلْوَاحَ ۖ وَفِى نُسْخَتِهَا هُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ هُمْ لِرَبِّهِمْ يَرْهَبُونَ

Maana

Na wakati ghadhabu ilipomtulia Musa, akazichukua mbao zile. Na katika maandiko yake kuna uongofu na rehema kwa wale ambao wanamhofu Mola wao Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Musa ilipo mtulia ghadhabu aliziokota zile mbao. Na katika maandiko yake mna uwongofu na rehema kwa wanao mwogopa Mola wao Mlezi. [154]

[154] Na Musa zilipo muondoka ghadhabu kwa kutoa udhuru nduguye, akazirejea zile mbao alizo ziweka chini akazichukua. Na kwenye hizo mbao umeandikwa uwongofu, na uwongozi, na njia za kupata rehema, kwa wale wanao iogopa ghadhabu ya Mola wao Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Zilipotulia hasira za Mûsã alizichukua mbao baada ya kuwa alizitupa chini, na ndani yake mlikuwa na maelezo ya haki na rehema kwa wanaomcha Allah Mtukufu na kuogopa mateso Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net