Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 151

Al-A'raaf 7:151

الأعراف

قَالَ رَبِّ ٱغْفِرْ لِى وَلِأَخِى وَأَدْخِلْنَا فِى رَحْمَتِكَ ۖ وَأَنتَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ

Maana

(Musa) akasema: Mola wangu Mlezi! Nifutie dhambi mimi na kaka yangu, na utuingize katika rehema yako. Nawe ni Mwenye kurehemu zaidi kuliko wote wenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Musa) akasema: Mola Mlezi wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu, na ututie katika rehema yako. Nawe ni Mwenye kurehemu kushinda wote wenye kurehemu. [151]

[151] Musa alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nisamehe kwa haya niliyo mfanyia ndugu yangu kabla sijayajua mambo. Na msamehe ndugu yangu ikiwa kakosea katika kushika pahala pangu kwa vizuri. Na tuingize katika eneo la rehema yako, kwani Wewe ndiwe Mwenye rehema nyingi kushinda wote wenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mûsã Alisema, ulipomfunukia udhuru wa ndugu yake na kujua kuwa yeye hakufanya uzembe katika kusimama imara juu ya amri ya Allah Mtukufu, «Mola wangu nisamehe ghadhabu zangu na umsamehe ndugu yangu yaliyopita kati yake na Wana wa Isrãîl, na ututie ndani ya rehema yako kunjufu, kwani wewe una huruma na sisi zaidi kuliko kila mwenye huruma».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net