Al-A'raaf 7:152
الأعرافإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ ٱلْعِجْلَ سَيَنَالُهُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَذِلَّةٌ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُفْتَرِينَ
Hakika wale waliojifanyia (na kumuabudu) ndama, itawapata ghadhabu kutoka kwa Mola wao Mlezi, na udhalilifu katika maisha ya dunia. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wazuao uongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale walio muabudu ndama, itawapata ghadhabu ya Mola wao Mlezi na madhila katika maisha ya dunia. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wazushi. [152]
[152] Hakika wale walio endelea kumfanya ndama kuwa mungu, kama Msamaria na wenziwe, itawafika ghadhabu kubwa kutoka kwa Mola wao Mlezi huko Akhera, na uvunjifu mkubwa katika maisha ya duniani. Na mfano wa malipo hayo ndio tunamlipa kila mwenye kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo, na akaabudu kinginecho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale waliomfanya ndama ni mungu itawapata wao ghadhabu kali kutoka kwa mola wao na unyonge katika uhai wa kilimwengu, kwa sababu ya kumkanusha kwao Mola wao. Na kama tulivyofanyia hawa, tutawafanyia wazushi wenye kuleta uzushi katika Dini ya Allah Mtukufu; na kila mwenye uzushi katika Dini ni mnyonge.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net