Al-A'raaf 7:145
الأعرافوَكَتَبْنَا لَهُۥ فِى ٱلْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَىْءٍ مَّوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَىْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا۟ بِأَحْسَنِهَا ۚ سَأُو۟رِيكُمْ دَارَ ٱلْفَـٰسِقِينَ
Na tukamuandikia kwenye mbao zile katika kila kitu, mawaidha na maelezo ya kina ya kila kitu. (Tukamwambia): Basi yachukue kwa nguvu na uwaamrishe kaumu yako wayachukue kwa ubora wake. Nami nitawaonyesha makazi ya wale waliovuka mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya mambo yote. (Tukamwambia): Basi yashike kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike kwa ubora wake. Nami nitakuonyesheni makaazi ya wapotofu. [145]
[145] Na tulimbainishia Musa katika zile mbao za Taurati kila kitu kilicho khusu mawaidha na hukumu zilizo elezwa mbali mbali, wanazo hitajia watu duniani na Akhera. Na tukamwambia: Zishike hizi mbao baraabara na kwa kuazimia. Na waamrishe watu wako washike yaliyo bora humo, kama kusamehe badala ya kulipiza kisasi, na kuachilia badala ya kungojea, na kulegeza badala ya kukaza. Enyi kaumu ya Musa! Nitakuonyesheni katika vitabu vyenu makaazi ya wale wanao asi amri za Mwenyezi Mungu, na watavyo angamia, ili mpate kuzingatia. Basi msende kinyume yakakusibuni yalio wasibu hao waasi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tulimuandikia Mûsã katika Taurati mawaidha ya kila anachokihitajia katika hukumu za Dini yake, ili yapatikane makemeo na mazingatio, na maelezo yanayofafanua mambo ambayo walikalifishwa nayo ya halali na ya haramu, maamrisho na makatazo, visa, mambo ya itikadi, habari na mambo yasiyoonekana. Allah Mtukufu Alimwambia, «Basi yashike kwa nguvu.» Yaani, ishike Taurati kwa kwa bidii na hima. «Na uwaamrishe watu wako wazitumie sheria za Allah Mtukufu zilizomo humo. Hakika mwenye kushirikisha miongoni mwao na wengineo, mimi nitamuonesha huko Akhera nyumba ya waasi, nayo ni Moto wa Allah Mtukufu ambao Ameutayarisha kwa maadui Wake waliotoka nje ya utiifu Wake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net