Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 144

Al-A'raaf 7:144

الأعراف

قَالَ يَـٰمُوسَىٰٓ إِنِّى ٱصْطَفَيْتُكَ عَلَى ٱلنَّاسِ بِرِسَـٰلَـٰتِى وَبِكَلَـٰمِى فَخُذْ مَآ ءَاتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ

Maana

(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Hakika Mimi nilikuteua uende kwa watu na jumbe zangu na maneno yangu. Basi chukua hayo niliyokupa na kuwa katika wanaoshukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteuwa wende kwa watu na Ujumbe wangu na maneno yangu. Basi chukua niliyo kupa na uwe katika wanao shukuru. [144]

[144] Mwenyezi Mungu alipo mzuilia Musa asimwone, akaingia kumhisabia neema zake ili amliwaze kwa vile kumkatalia, akamwambia: Ewe Musa! Mimi nimekufadhilisha, na nimekuteua kuliko watu wote wa zama zako, ili ufikishe vitabu vya Taurati, na kwa kusema nawe bila ya kuwapo mtu kati. Basi yashike hayo niliyo kukufadhili, na unishukuru kama wafanyavyo wenye kushukuru, wanao kadiri neema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Akasema, Ewe Mûsã, Mimi nimekuchagua kati ya watu kwa ujumbe wangu kwa viumbe wangu niliokutuma kwao na kwa kusema kwangu na wewe pasi na mtu wa kati. Basi chukua niliyokupa kati ya maamrisho yangu na makatazo yangu, ushikamane nayo na uyatumie na uwe ni miongoni mwa wenye kumshukuru Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa utume aliokupa na Akakuhusu kwa maneno Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net