Al-A'raaf 7:126
الأعرافوَمَا تَنقِمُ مِنَّآ إِلَّآ أَنْ ءَامَنَّا بِـَٔايَـٰتِ رَبِّنَا لَمَّا جَآءَتْنَا ۚ رَبَّنَآ أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ
Nawe hutushutumu kwa chuki isipokuwa kwa kuwa tumeziamini Ishara za Mola wetu Mlezi pindi zilipotujia. Ewe Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira na utufishe hali ya kuwa ni Waislamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nawe hukuudhika nasi ila kwa kuwa tumeziamini Ishara za Mola Mlezi wetu zilipo tujia. Ewe Mola Mlezi wetu! Tumiminie uvumilivu na utufishe hali ni Waislamu. [126]
[126] Na wewe hutuchukii na kutuadhibu ila kwa kuwa tumemsadiki Musa, na tumezikubali zilipo tujia Ishara za Mola wetu Mlezi zilio wazi, zenye kuonyesha Haki! Kisha wakamuelekea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu, wakisema: Ewe Mola Mlezi wetu! Tumiminie subira kubwa, itupe nguvu kuhimili shida zote; na utufishe katika Uislamu bila ya kuteseka kwa anayo tuahidi Firauni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wewe hukutupata na jambo lolote la kutuaibisha na kutupinga kwalo, ewe Fir‛awn, isipokuwa ni kule kuamini kwetu na kukubali kwetu hoja za Mola wetu na dalili Zake alizokuja nazo Mûsã ambazo wewe huwezi kuleta mfano wake wala yoyote mwingine asiyekuwa Allah Mtukufu Ambaye ni Yake mamlaka ya mbingu na ardhi. Mola wetu! Tumiminie subira kubwa na uthabiti juu yake, na utufishe tukiwa ni wenye kufuata amri yako, wenye kumfuata Mtume wako.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net