Al-A'raaf 7:127
الأعرافوَقَالَ ٱلْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُۥ لِيُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَ ۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَآءَهُمْ وَنَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَـٰهِرُونَ
Na wakasema waheshimiwa kutoka kwa kaumu ya Firauni: Je, unamuacha Musa na kaumu yake ili wafanye uharibifu katika ardhi na akuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawaua sana wavulana wao, na tuwaache hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Unamuacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na wakuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawauwa wavulana wao, na tutawaacha hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao. [127]
[127] Baada ya Firauni na watu wake kuona waliyo yaona, katika vile kudhihiri mambo ya Musa na nguvu za ushindi wake, na wachawi wakamuamini, walisema wakuu wa kaumu yake: Unamuacha Musa na watu wake wawe huru katika amani, ili mwisho wao wawafisidi kaumu yako dhidi yako katika nchi ya Misri kwa kuwatia katika dini yao, na wakuache wewe na miungu yako bila ya wao kujali? Hapo watu wa Misri watakuona wewe na hiyo miungu kuwa mmeshindwa. Firauni akasema kuwajibu: Tutawawauwa watoto wao wa kiume wa watu hawa, kila anaye zaliwa; na tutawabakisha wa kike wawe hai, ili wasiwe na nguvu, kama tulivyo fanya zamani. Na sisi tuko juu yao kwa kuwashinda na kwa utawala, na kuwafanyia kahari.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakubwa miongoni mwa watu wa Fir‛awn walisema kumwambia Fir‛awn, «Unamuacha Mûsã na watu wake, Wana wa Isrãîl, wawaharibu watu katika nchi ya Misri kwa kuwageuzia dini yao na kuwaletea ibada ya Allah Mtukufu Peke Yake, Asiye na mshirika, na kuacha kukuabudu wewe na kuwaabudu waungu wako?» Fir‛awn akasema, Tutawaua watoto wa kiume wa Wana wa Isrãîl, na tutawaacha watoto wao wa kike waishi ili watumike; na sisi tuko juu yao kwa nguvu za ufalme na mamlaka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net