Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 125

Al-A'raaf 7:125

الأعراف

قَالُوٓا۟ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ

Maana

Wakasema: Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. [125]

[125] Nao hawakuibali kauli yake wala vitisho vyake, kwa kuwa Imani ilikwisha saki ndani ya nyoyo zao. Wakamwambia: Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. Kwa hivyo tunaneemeka katika rehema yake na bora ya malipo yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walisema wachawi kumwambia Fir‛awn, Tuna uhakika kwamba sisi ni wenye kurejea kwa Allah Mtukufu na kwamba adhabu Yake ni kali zaidi kushinda adhabu yako. Tutasuburi kikwelikweli leo kwa adhabu yako, tupate kuokoka na adhabu ya Allah Mtukufu Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net