Al-A'raaf 7:124
الأعرافلَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَـٰفٍ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ
Lazima nitaikata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha. Kisha lazima nitawasulubisha nyote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lazima nitaikata mikono yenu na miguu yenu mbali mbali. Kisha nitakutundikeni misalabani. [124]
[124] Na ninakuapieni kuwa nitakuteseni vikali, na nitakukateni mikono yenu na miguu yenu mbali mbali, nitakata mkono wa upande mmoja na mguu wa upande wa pili, kisha nitakutundikeni misalabani, kila mmoja wenu, nanyi mmo katika hali hiyo, ili muwe ni zingatio kwa anaye jifikiria kutufanyia vitimbi, au kutaka kuufanyia uasi utawala wetu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Nitaikatakata mikono yenu na miguu yenu, enyi wachawi, kwa kupishana: kwa kuukata mkono wa kulia na mguu wa kushoto au mkono wa kushoto na mguu wa kulia, kisha nitawatungika nyinyi nyote juu ya vigogo vya mitende kwa njia ya kuwatesa na ili kuwafanya watu watishike.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net