Al-A'raaf 7:123
الأعرافقَالَ فِرْعَوْنُ ءَامَنتُم بِهِۦ قَبْلَ أَنْ ءَاذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَمَكْرٌ مَّكَرْتُمُوهُ فِى ٱلْمَدِينَةِ لِتُخْرِجُوا۟ مِنْهَآ أَهْلَهَا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ
Akasema Firauni: Mmemuamini kabla mimi kuwapa idhini? Hakika, hii ni njama mliyoipangia huko mjini ili muwatoe humo wenyewe. Basi karibu mtajua!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema Firauni: Mmemuamini kabla sijakupeni idhini? Hizi ni njama mlizo panga mjini mpate kuwatoa wenyewe. Lakini karibu mtajua! [123]
[123] Jambo hili lilimtisha Firauni na ikafoka ghadhabu yake, akasema: Hivyo nyinyi mmemuamini na kumsadiki Mola Mlezi wa Musa na Haarun kabla sijakupeni ruhusa mimi? Hakika hapa pana kijambo mmekizua nyinyi na Musa na Haarun kwa kuwafikiana. Na haya si chochote ila ni vitimbi mlivyo vipanga katika mji wa Misri mpate kuwatoa wenyewe kwa hila yenu. Basi ngojeni, mtaiona adhabu itayo kushukieni kuwa ndio jaza yenu kwa kumfuata Musa na Haarun, na ndio adabu yenu kwa hivi vitimbi vyenu na khadaa!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Fir‛awn akasema kuwaambia wachawi, «Mumemuamini Allah Mtukufu kabla sijawapa idhini mumuamini? Hakika kumuamini kwenu Allah Mtukufu, kumsadiki kwenu Mûsã na kuukubali kwenu unabii wake ni hila mlizozipanga nyinyi na Mûsã ili muwatoe watu wa mji wenu kutoka humo, na ili muzivamie heri zake na mfaidike nazo peke yenu.Basi mtajua, enyi wachawi, adhabu na mateso yatakayowashukia nyinyi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net