Al-A'raaf 7:117
الأعرافوَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَإِذَا هِىَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ
Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Itupe fimbo yako, na tazama, ikawa inavimeza vyote vile walivyovizulia uongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Tupa fimbo yako. Mara ikavimeza vyote vile walivyo vibuni. [117]
[117] Mwenyezi Mungu akaitoa amri yake kumpelekea Musa: Tupa fimbo yako. Sasa umekwisha fika wakati wake. Akaitupa kama alivyo amrishwa. Mara hiyo fimbo ikaingia kuvimeza vile vizushi vyao walivyo zua na kubuni!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo Allah Mtukufu Alimletea wahyi mja Wake na Mtume Wake Mûsã, amani imshukiye, katika kisimamo hicho kikubwa ambacho hapo Allah Mtukufu Alipambanua baina ya ukweli na urongo, akimuamuru akitupe kilichoko kwenye mkono wake wa kulia, nacho ni fimbo yake. Akaitupa na papo hapo ikawa inavimeza vile wanavyovitupa na kuwafanya watu wadhanie kuwa ni vya kweli na ilhali ni vya urongo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net