Al-A'raaf 7:116
الأعرافقَالَ أَلْقُوا۟ ۖ فَلَمَّآ أَلْقَوْا۟ سَحَرُوٓا۟ أَعْيُنَ ٱلنَّاسِ وَٱسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَآءُو بِسِحْرٍ عَظِيمٍ
Akasema: Tupeni! Basi walipotupa, waliyafanyia uchawi macho ya watu na wakawatia hofu, na wakaleta uchawi mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Tupeni! Basi walipo tupa waliyazuga macho ya watu na wakawatia khofu, na wakaleta uchawi mkubwa. [116]
[116] Musa akwajibu jawabu ya mwenye imani ya kushinda, akionyesha kutowabali: Tupeni nyinyi kwanza hicho mnacho tupa. Walipo tupa kila mmoja wao, navyo ni kamba na fimbo, macho ya watu yalizugwa, na ikawapitikia kuwa walicho kifanya kile ni hakika kweli. Na hali haikuwa ila ni kiini macho tu. Mambo yale yaliwatisha watu, na nyoyo zao zikaingia khofu na kitisho. Kwani wachawi wale waliwaletea watu uchawi unao onekana ni mkubwa, na athari yake katika macho yao ni kubwa!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akasema Mûsã kuwaambia wachawi, «Tupeni nyinyi.» Walipotupa kamba na fimbo, waliyaroga macho ya watu yakaona kwamba yale waliyoyafanya ni ya kweli, na hali yalikuwa ni kiinimacho na vitu vya kudhania, na waliwatisha watu vitisho vikali na walikuja na uchawi wa nguvu ulio mwingi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net