Al-A'raaf 7:115
الأعرافقَالُوا۟ يَـٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلْقِىَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ نَحْنُ ٱلْمُلْقِينَ
Wakasema: Ewe Musa! Ima utupe wewe, au tuwe sisi ndio watupao?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Ewe Musa! Je, utatupa wewe, au tutakuwa sisi tutao tupa? [115]
[115] Kisha wachawi wakamgeukia Musa, baada ya Firauni kuwaahidi alivyo waahidi, na wao wakaonyesha wana imani na nafsi zao na kujitayarisha kwao kwa uchawi wao katika uwanja wa mapambano. Wakamwabia: Ama utupe ulicho nacho kwanza, au sisi tuwe wenye kutupa tulicho nacho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakasema wachawi wa Fir‛awn kumwambia Mûsã, kwa njia ya kujiona na kutojali. «Ewe Mûsã, chagua uwe ni wa mwanzo kutupa fimbo yako au tuwe sisi ni wa mwanzo kutupa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net