Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 67 · Aya ya 28

Al-Mulk 67:28

الملك

قُلْ أَرَءَيْتُمْ إِنْ أَهْلَكَنِىَ ٱللَّهُ وَمَن مَّعِىَ أَوْ رَحِمَنَا فَمَن يُجِيرُ ٱلْكَـٰفِرِينَ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ

Maana

Sema: Mwaonaje, ikiwa Mwenyezi Mungu ataniangamiza mimi na wale walio pamoja nami, au akiturehemu, ni nani atakayewalinda makafiri mbali na adhabu chungu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mwaonaje, ikiwa Mwenyezi Mungu atanihiliki mimi na walio pamoja nami, au akiturehemu, ni nani atakaye walinda makafiri na adhabu chungu? [28]

[28] Sema: Nambieni, ikiwa Mwenyezi Mungu akinifisha mimi na Waumini walio pamoja nami, kama mnavyo tamani yawe, au akaturehemu akaakhirisha ajali yetu, na akatusamehe asituadhibu, maana itakuwa katuokoa katika hali zote mbili, basi nani atakaye wakinga makafiri na adhabu chungu wanayo istahiki kuipata kwa sababu ya ukafiri wao, na kudanganyika kwao na miungu yao?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, (ewe Mtume), uwaambie hawa makafiri, «mnaonaje, iwapo Allah Mtukufu Atanifisha pamoja na Waumini walio pamoja nami, kama mnavyotamani, au Ataturehemu avicheleweshe vipindi vyetu vya kufa na Atuepushie adhabu yake, hivi ni nani ambaye atawahami makafiri na aizuie adhabu kali yenye kuumiza isiwafikie?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mulk

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net