Al-Mulk 67:27
الملكفَلَمَّا رَأَوْهُ زُلْفَةً سِيٓـَٔتْ وُجُوهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَقِيلَ هَـٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تَدَّعُونَ
Lakini watakapoiona karibu, nyuso za wale waliokufuru zitahuzunishwa, na itasemwa: Hayo ndiyo mliyokuwa mkiyaomba mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini watakapo iona karibu, nyuso za walio kufuru zitahuzunishwa, na itasemwa: Hayo ndiyo mliyo kuwa mkiyaomba. [27]
[27] Watakapo yaona hayo yaliyo ahidiwa yapo karibu nao, nyuso za makafiri zitajaa huzuni na unyonge, na wataambiwa kwa kuwakejeli na kuwatia uchungu: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyataka yaje kwa haraka!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watakapoiona makafiri adhabu ya Allah Mtukufu ikiwa iko karibu nao na wakaishuhudia, utajitokeza unyonge na huzuni kwenye nyuso zao na hapo wataambiwa, kwa njia ya kuwalaumu na kuwakaripia, «Hii ndiyo ile mliokuwa mkitaka iharakishwe ulimwenguni».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net