Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 67 · Aya ya 29

Al-Mulk 67:29

الملك

قُلْ هُوَ ٱلرَّحْمَـٰنُ ءَامَنَّا بِهِۦ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ

Maana

Sema: Yeye ndiye Mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea. Basi mtakuja jua ni nani aliye katika upotovu ulio dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Yeye ndiye Mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea. Mtakuja jua ni nani aliye katika upotovu ulio dhaahiri. [29]

[29] Yeye huyo ndiye Arrahman, Mwingi wa Rehema, tunaye msadiki sisi, na nyinyi hamumsadiki. Yeye tu peke yake ndiye tunaye mtegemea, na nyinyi mnawategemea wenginewe. Mtakuja jua itakapo teremka adhabu ni kundi gani kati yetu lilio tengeka mbali na Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, «Ni Allah Mtukufu! Yeye Ndiye Mwingi wa rehema. Tumemuamini na tumeifuata Sheria Yake kivitendo na tumemtii. Na Kwake yeye, Peke Yake, tumetegemea katika mambo yetu yote. Basi mtajua, enyi makafiri, itakapoteremka adhabu, ni yupi kati ya makundi mawili miongoni mwetu: sisi na nyinyi, yuko mbali waziwazi na njia ya Allah Mtukufu iliyonyooka».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mulk

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net