Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 67 · Aya ya 17

Al-Mulk 67:17

الملك

أَمْ أَمِنتُم مَّن فِى ٱلسَّمَآءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

Maana

Au mnadhani mko salama kutokana na aliyeko juu ya kuwa Yeye hatakupelekeeni kimbunga chenye changarawe? Basi mtajua vipi maonyo yangu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au mnadhani mko salama kwa alioko juu ya kuwa Yeye hakupelekeeni kimbunga chenye changarawe? Mtajua vipi maonyo yangu? [17]

[17] Bali, mmejiaminisha na Mwenye Ufalme wa mbinguni, kuwa hatakupelekeeni upepo wa kukupopoeni kwa changarawe? Hapo basi mtakijiua kitisho cha onyo langu kwenu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au mmesalimika kuwa Allah Mtukufu Aliye juu ya mbingu Hatawatumia upepo wenye kuwapiga mawe madogomadogo? basi mtajua, (enyi makafiri), kua likoje onyo langu kwenu mnapoiona adhabu. Na huko kujua wakati huo hakutawanufaisha. Katika hii aya pana kuthibitisha kuwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Yuko juu kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake, kutakasika ni Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mulk

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net