Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 67 · Aya ya 16

Al-Mulk 67:16

الملك

ءَأَمِنتُم مَّن فِى ٱلسَّمَآءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ ٱلْأَرْضَ فَإِذَا هِىَ تَمُورُ

Maana

Je, mmesalimika kutokana na aliyeko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mnadhani mko salama kwa alioko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika! [16]

[16] Je! Mmejiaminisha na Mwenye Ufalme wa mbinguni, kuwa hatakukatieni ardhi, akakuchukulieni kwa ghafla kwa mtikiso mkubwa?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je mmesalimika, (enyi makafiri wa Makkah), na Allah Mtukufu Aliye mbinguni kuwa Hatawadidimiza ardhini ikawa inatetemeka na nyinyi mpaka mkaangamia?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mulk

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net