Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 67 · Aya ya 18

Al-Mulk 67:18

الملك

وَلَقَدْ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ

Maana

Na bila ya shaka walikwisha kanusha wale waliokuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na bila ya shaka walikwisha kanusha walio kuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu? [18]

[18] Na hakika walikwisha wakanusha Mitume wao hao walio kuwa kabla ya kaumu yako. Basi ghadhabu yangu juu yao ilikuwa hali gani kwa nilivyo waangamiza na kuwashika!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika walikanusha wale waliokuwa kabla ya makafiri wa Makkah kama vile watu wa Nûḥ, ‛Ᾱd na Thamūd walivyowakanusha Mitume wao. Basi kulikuwa namna gani kule kuwakasirikia kwangu na kuwageuzia kwangu neema waliyokuwa nayo kwa kuwateremshia adhabu na kuwaangamiza?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mulk

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net