At-Tahrim 66:9
التحريميَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ جَـٰهِدِ ٱلْكُفَّارَ وَٱلْمُنَـٰفِقِينَ وَٱغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ
Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki, na kuwa mgumu kwao! Na makazi yao ni Jahannamu. Na hayo ni marejeo mabaya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na kuwa mgumu kwao! Na makaazi yao ni Jahannamu. Na hayo ni marejeo mabaya. [9]
[9] Ewe Nabii! Pambana kwa Jihadi na hao walio tangaza ukafiri wao, na wanaafiki walio uficha ukafiri wao, kwa kila unacho kimiliki, nguvu na hoja. Na kuwa mkali juu ya makundi yote mawili hayo katika Jihadi yako. Na makaazi ya hao ni Jahannamu. Na marejeo maovu ni hayo marejeo yao!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Pigana jihadi na wale waliouonyesha ukafiri waziwazi na wakautangaza, na pigana nao kwa upanga, na pigana jihadi na wale waliouficha ukafiri kwa hoja na kwa kusimamisha hukumu za Sheria na alama za Dini. Na utumie ukali na ugumu katika kupigana jihadi na makundi mawili hayo. Na makazi yao ambayo watakwenda kukaa huko Akhera ni moto wa Jahanamu. Na ni marejeo maovu mno hayo watakayoyarejea!
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net